SUMMARY OF THE RULES OF CAMELOT

In the Swahili Language

 

Text and Diagrams © 1999-2009 Michael Wortley Nolan and the World Camelot Federation

Translation courtesy of Eli Kern

 

(Please note that what follows is the translation of a general summary of Camelot rules; it is not a translation of the World Camelot Federation Official Rules of Camelot.)

 

Camelot huchezwa kati ya wapinzani wawili wanaocheza kila nafasi mengine kwenye kibao cha miraba 160.  Kila mchezaji hulinda Ngome ambayo ni miraba miwili kwenye upande wake wa kibao.  Kila mchezaji huanza mchezo na vipande 14:  Askari wa Farasi wanne na Wanaume kumi. 

 

 

Mwanzoni

 

Kuna aina nne za tendo:

 

1. Tendo la Kawaida: Kipande kimoja (Askari wa Farasi au Mwanaume) huruhusiwa kusogea mraba moja upande wowote kufika mraba tupu wa karibu. 

 

 

Tendo la Kawaida

 

2. Matiti: Kipande kimoja (Askari wa Farasi au Mwanaume) huruhusiwa kuruka upande wowote juu ya kipande kingine cha mwenyewe ambacho kiko mraba karibu kufika mraba tupu karibu na kipande hicho.  Vipande ambavyo viko chini ya kipande kilichoruka bado ni salama kwenye kibaoni.  Mchezaji huruhusiwa kuruka juu ya vipande vingi katika tendo moja.  Mchezaji hairuhusiwi kuanza na kuisha kwenye mraba sawa.  Mchezaji haihitaji kamwe kuruka.   

 

                       

Matiti                                                         Baada ya Matiti

 

3. Kuruka:  Kipande kimoja (Askari wa Farasi au Mwanaume) huruhusiwa kuruka upande wowote juu ya kipande cha mpinzani ambacho kiko mraba karibu kufika mraba tupu karibu na kipande hicho.  Vipande vya mpinzani ambavyo viko chini ya kipande kilichoruka huondolewa.  Ni lazima mchezaji aruke kama kipande kimoja chake kiko karibu na kipande bila kinga cha mpinzani.  Ukiruka juu ya kipande kimoja, ni lazima uendelee kuruka kama kipande chako kimefika mraba karibu na kipande kingine bila kinga cha mpinzani.  Mchezaji huruhusiwa kuchagua kipande kipi aondoe, halafu achague ni kipande chake kipi kitaruka.  Kama mchezaji ahitaji kuruka, anaweza kufanya Shambulio la Askari ya Farasi baadala ya Kuruka.  Mchezaji hahitaji kuruka kama, katika ya tendo lililopita, aliruka kipande chake juu ya kipande cha mpinzani kufika Ngome ya mwenyewe.  

 

                       

Kuruka                                                    Baada ya Kuruka

 

4. Shambulio la Askari wa Farasi:  Askari wa Farasi huruhusiwa kufanya Matiti pamoja na Kuruka katika ya tendo moja.  Ukitumia Shambulio la Askari wa Farasi ni lazima kwanza ufanye Matiti kabla ya Kuruka.  Askari ya Farasi haihitaji kamwe kufanya Shambulio la Askari wa Farasi.  Kama baada ya kufanya Matiti wa Askari wa Farasi, kipande hiki kiko karibu na kipande cha mpinzani unachoweza kuruka, ni lazima uruke isipokuwa katika ya tendo hili Askari wa Farasi hiki kitachuka kipande kingine cha mpinzani mahali pengine.  Kama Askari wa Farasi anaruka juu ya kipande kimoja cha mpinzani, ni lazima aendelee kuruka kama amefika karibu na kipande kingine bila kinga cha mpinzani. 

 

                                   

 

Shambulio la Askari wa Farasi                           Baada ya Shambulio la Askari wa Farasi

 

Mchezaji hairuhusiwi kufanya Tendo la Kawaida au Matiti kwaajili ya kufika Ngome ya mwenyewe.  Mchezaji huruhusiwa kuruka, au kuruka katika ya Shambulio la Askari wa Farasi, kwaajili ya kufika Ngome ya mwenyewe.  Kama mchezaji akiruka Ngomeni ya mwenyewe, ni lazima aruke tena kutoka Ngome kwake ikiwezekana.  Mchezaji aliyeruka ndani ya Ngome ya mwenyewe, ni lazima katika ya tendo lijalo aondoke Ngomeni ya mwenyewe.  Mchezaji anayeondoka Ngome ya mwenyewe ni lazima aruke ikiwezekana baadala ya kutumia Tendo la Kawaida au Matiti. 

 

Kipande kilichoingia Ngome ya mpinzani hakiruhusiwi kuondoka, lakini huruhusiwa kusogea mraba mwingine wa Ngome hiyo.  Mchezaji ana Tendo la Ngome mbili tu katika ya mchezo wote. 

 

Mchezaji huweza kushinda kutumia jinsi tatu tofauti:

 

1. Mchezaji anasogeza vipande viwili ndani ya Ngome ya mpinzani.

 

 

Nyeupe ameshinda kupitia kusogeza vipande viwili ndani ya Ngome ya Nyeusi.

 

2. Mchezaji anachukua vipande vyote vya mpinzani halafu vipande vyake viwili au zaidi bado viko kibaoni.

 

 

Nyeupe ameshinda kupitia kuchukua vipande vyote vya Nyeusi.

 

3. Mchezaji ana vipande viwili au zaidi halafu mpinzani haiwezi kufanya tendo lolote.

 

 

Nyeupe ameshinda kwasababu Nyeusi haiwezi kufanya tendo lolote.

 

Hutoka sare kama wachezaji wote wana kipande kimoja tu. 

 

 Imetoka sare.